MSHAMBULIAJI Diego Costa amesema kwamba kwa sasa anajiandaa kuondoka Chelsea baada ya kuambiwa na kocha Antonio Conte hahitajiki kwenye klabu.
Costa amesema Conte amemtumia ujumbe wa maandishi kwenye simu akimuambia kwamba hamtaki tena katika klabu na sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kuondoka Stamford Bridge kurejea Atletico Madrid, lakini adhabu ya zuio la kusajili kwa klabu yake hiyo ya zamani ndiyo kikwazo.
Chelsea inamtaka mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, ambaye yuko tayari kurejea klabu yake ya zamani na wako tayari kumuuza Costa ili kuongezea fedha katika dau la Pauni Milioni 100 zinazotakiwa.
Diego Costa amesema ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu na Antonio Conte kumuambia hamhitaji tena Chelsea.
Timu ya zamani ya Costa, Atletico Madrid iko tayari kumrejesha shujaa wake, lakini wamefungiwa kusajili wachezaji wapya hadi Januari 2018.
Na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania, Costa atalazimika kuangalia ofa nyinginem baada ya kutofautiana na Conte mwezi Januari juu ya mchezaji huyo kutikuwa fiti jwa mchezo.
Lakini pia mchezaji huyo amekuwa akitakiwa Tianjin Quanjian ya Ligi Kuu ya China, ingawa mwenyewe amekuwa akisema wakati wote ataipa uzito ofa ya kurejea Atletico.
Chapisha Maoni