0
Mabingwa wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara Timu ya Soka ya Yanga wameaga michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kutolewa na mabingwa wa zamani wa Kenya AFC Leopards kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa Marselas Ingotsi, lakini mlinda mlango wa AFC Leopards, Ian Otieno naye akacheza mikwaju ya Said Mussa na Said Juma ‘Makapu’.
Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo mshambuliaji Mzambia, Obrey Chira ndiyo pekee walifunga penati za Yanga, wakati Bernard Mango, Allan Katerega, Duncan Otieno na Ian Otieno wakafunga za AFC Leopards.
Dakika 90.
Katika dakika 90 za kawaida za mchezo, timu zote zilimiliki mpira sawa, ingawa hakukuwa na mashambulizi ya kushitua, huku mchezo ukiwa wa nguvu kwa dakika zote hali iyofanya mchezo huo kuwa na faulo nyingi hasa dakika 30 za mwanzo.
Allan Kateregga wa AFC Leopards alipiga shuti kali dakika ya 39, lakini kipa wa Yanga, Dida akadaka. Kiungo chipukizi wa Yanga, Yussuf Mhilu alipiga shuti zuri dakika ya 43, lakini beki wa AFC Leopards, Joshua Mawira akaokoa.
AFC Leopards wakapoteza nafasi nyingine baada ya Vincent Oburu kushindwa kutumia pasi ya Ingotsi kwa kupiga shuti dhaifu lililodakwa na Dida. Chirwa naye akapiga krosi nzuri dakika ya 60, lakini mpira ukatoka nje.
Chipukizi Maka Edward Mwakalukwa naye akapiga nje dakika ya 62 baada ya kupokea pasi ya Juma Mahadhi.
SOMA: AFC Leopards." target="">Super Cup: Yanga wataka kumaliza shughuli mapema dhidi ya AFC Leopards.
Kufuatia Ushindi huo AFC Leopards watakutana na mshindi wa Mchezo kati ya Nakuru All Stars na Gor Mahia ambapo kama atakutana na Mtani wake Gor Mahia utakuwa mchezo wa kwanza wa watani hao kufanyika nje ya Kenya toka mwaka 1985 walipocheza nchini Sudan kwenye michuano ya CECAFA Ngazi ya Vilabu ambapo AFC Leopards waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Chapisha Maoni

 
Top