0
Kipa namba moja wa Chelsea, Thibaut Courtois ametikisa kiberiti akitaka mshahara wake wa Pauni 90,000 kwa wiki uongezwe mara mbili.
Klabu yake, Chelsea ilikuwa na matumaini ya kuongeza msaada kwa kipa Thibaut Courtois unaoendelea hadi 2019.
Nyota huyo wa Ubelgiji amekuwa akidai apewe mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki, huku maofisa wa klabu hiyo wakiwa na matumaini kuwa mwafaka utafikiwa ili aendelee kuichezea msimu ujao.
Pande hizo mbili zimekuwa zikiendelea na mazungumzo ambako Courtois amesema mazungumzo yamesimama kwa sasa.
Nyota mwenzake wa Ubelgiji, Eden Hazard analipwa Pauni 200,000, sawa na kipa wa Manchester United, David De Gea .
Kocha Antonio Conte amekuwa na matumaini ya kuendelea kubaki na kipa wake chaguo la kwanza.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top