Uongozi wa Klabu ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es salaam umewaziba mdomo wale Wote wanaosema kwamba klabu hiyo inafanya Usajili kwa lengo la kuwakomoa majirani zao Dar Young Africans.
Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu, amesema kamati ya Usajili inafanyakazi kutokana na ripoti ya Mwalimu Joseph Omog, na Si kwa hulka zao wenyewe na kila anayesajiliwa ana baraka kutoka katika Benchi la Ufundi la Timu yao.
-Mwalimu ameacha ripoti yake ambayo sisi tunaifahamu na Ndio tunayotumia kwa Usajili, sasa huyo anayesema pembeni kwamba Simba inasaini kwa maelekezo ya Nje ya ripoti ya Omog sasa aje atuambie kama anayo hiyo ripoti" Amesema.
Ni Wazushi.
Kaburu amewaita wale Wote wanaosambaza taarifa Ya kwamba wanafanya Usajili wa kuwakomoa wengine ni wazushi ambao Hawajui lolote kuhusu klabu yao.
-Haya ni Maneno ya kuzusha tu tena na watu ambao hawaujui Mpira kwa sidhani kama Nina muda wa kuanza kubishana nao, Ila tu kwa kifupi uongozi Upo makini na Unajua unataka nini lengo ni kupata timu bora msimu ujao" Kaburu aliongeza.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.