0
Klabu ya Azam Maarufu kama Wanarambaramba imewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa hawatawaondoa wachezaji wao wa Kigeni Licha ya fumuafumua ya kikosi inayoendelea hivi sasa.
Kwa niaba ya Klabu hiyo Afisa Habari Jaffary Idd Maganga amewahakikishia Mashabiki Hao kuwa bado wanamikataba na wachezaji wao wa kimataifa na hawana kusudio lolote la kuvunja Mikataba yao.
-Watu wengi sana wamekuwa wakiuliza kuhusu wachezaji wetu wa kimataifa, niwatoe Wasiwasi tu kuwa bado tunaendelea nao hakuna ambaye tutamuacha" Amesema Maganga.
Usajili ujao.
Maganga ameongeza kuwa Licha ya kuendelea kuwa nao Lakini watakaa na kupitia Mikataba yao pamoja na Mchango wao kwa timu ili wajue nini watafanya katika Dirisha dogo la Usajili Lakini si kwasasa Kwani Wote wanahitajika na wanamikataba halali.
Baadhi ya wachezaji wa Kigeni wa Azam FC ni Samuel Afful, Yahaya Mohammed, Bruce Kangwa, Daniel Amouh, Yakubu Mohammed na Stephan Kingue Mpondo.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top