0
 Kuna kila dalili kwamba Mohamed Salah anarudi Ligi Kuu England akitokea AS Roma.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea anatajwa kutua Liverpool kesho kwa uchunguzi
wa afya yake baada ya klabu yake, Roma kukubali ofa ya Pauni 39 milioni.
Metro Sport limeeleza kuwa ofa hiyo ya Liverpool imekubaliwa na Jumanne, Salah atafanyiwa uchunguzi wa afya yake, gazeti hilo limenukuu taarifa kutoka Misri.
Jumamosi, mchezaji huyo alieleza kocha Jurgen Klopp alikuwa amewasilisha ofa ya Pauni 39.4 milioni kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 25.
Mtandao wa KingFut ulieleza ofa hiyo imekubaliwa na klabu hiyo, AS Roma baada ya majadiliano na wakala wake, Ramy Abbas, jijini London.

Chapisha Maoni

 
Top