Dar es Salaam. Upangaji wa makundi na ratiba ya mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup 2017 umefanyika jijini jioni hii.
Katika droo hiyo iliyofanyika kwenye ufukwe wa Escape One jijini, mabingwa watetezi, Temeke Market wameangukia kundi G sambamba na timu za Stimu Tosha, Makuburi na Dar es Salaam Police College.
Akizungumza wakati wa hafla ya upangaji makundi hayo, mkurugenzi wa mashindano hayo Shaffih Dauda alisema kuwa ufunguzi wa hatua hiyo utaanza Juni 17 kwenye Uwanja wa Kinesi kati ya timu za Makuburi na Stimu Tosha.
"Droo hii imehusisha jumla ya timu 32 ambazo zimepangwa kwenye makundi nane yenye timu nne kila moja.
"Tunaamini mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na maandalizi ambayo timu zote 32 zimeyafanya, " alisema Dauda.
Chapisha Maoni