0
Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, Peter Kadutu, Ayoub Nyenzi amechukua fomu za kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Uchaguzi wa TFF utafanyika Agosti 12, Mkoani Dodoma kwa wajumbe wa mkutano mkuu watamchagua rais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Kadutu ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora anagombea ujumbe kupitia kanda ya Tabora na Kigoma wakati mjumbe wa kamati ya utendaji anayewakilisha mikoa ya Iringa na Njombe, Nyenzi anatetea nafasi yake.
Mbunge Kadutu alisema ameamua kujitokeza kuwania nafasi hiyo ili aongeze ufanisi katika maendeleo ya mpira wa miguu.
"Watu wengi huwa wanazitazama nafasi za urais wa shirikisho na makamu wake, lakini kiuhalisia kamati ya utendaji ndio yenye nguvu ya kiuamuzi na uendeshaji ya mchezo wa soka.
Binafsi nimeamua kujitokeza kuwania nafasi hii nikiamini kuwa nitapata fursa ya kutoa ushauri kwa rais na viongozi wenzangu ili kuhakikisha soka letu linapiga hatua," alisema Kadutu.
Mapema juzi, Rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi sambamba na makamu wake Wallace Karia na mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Iman Madega walijitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais.
Wakati Godfrey Nyange 'Kaburu' na Michael Wambura walichukua fomu za kuwania nafasi ya umakamu wa rais, huku Mulamu Ng’ambi akitarajiwa kuchukua fomu wakati wowote kutoka sasa.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top