0
Ndoto ya nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney kupata timu mpya ya kuchezea msimu ujao imeingia doa baada ya klabu mbalimbali kutishwa na ukubwa mshahara wake.
Rooney ambaye ameshindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kocha Jose Mourinho amekuwa akitaka kuihama klabu hiyo.
Lakini, mshahara wake wa Pauni 300,000 kwa wiki unazifanya klabu nyingi ziogope kuzungumza naye.
Kwa sababu hiyo, Rooney amekwama kwenye klabu hiyo ya Old Trafford baada ya kukosa mahali ambako atauzwa kwa bei ndogo kuliko inayotakiwa na Manchester United.
Hadi sasa, Rooney, 31, ana mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake, anasubiri huruma ya United kupunguza bei ili kumwezesha kupata mahali pa kwenda. Kinyume chake, atabaki Old Trafford bila kucheza na kuondoka akiwa mchezaji huru.
Klabu ya Everton chini ya kocha Ronald Koeman imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji huyo aliyekulia Goodison Park.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top