0
Wakati Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi akihusishwa na Kujiunga na Miamba ya soka ya Tanzania Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam,Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu ameibuka na kusema kuwa Watu wawe watulivu kwani mazungumzo yanaendelea.
Kaburu amesema suala la kuonekana Tanzania kwa Mshambuliaji huyo ni kweli lakini bado wapo katika mazungumzo na kwamba Muda pekee ndio utakaozungumza kuhusiana na Uhamisho wa Mchezaji huyo.
-Muda bado upo tutakapokamilisha yote basi tutawatambulisha, ni jambo la kufanyia kazi si la kukurupuka, nawaomba sana wapenzi wa Simba kuwa na Subira kwani siwezi kuongelea mchakato ulivyo nitazungumza mambo yote yakikamilika” Alisema Kaburu.
Okwi katika Twitter.
Wakati hayo yakijiri Mshambuliaji mwenyewe ameibuka katika Mtandao wake wa Twitter na kuandika kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili.
Okwi ameandika ‘ Contrary to reports that I have rejoined Simba SC, I would like to let you al know that no agreement has been reached yet!!’
akimaanisha kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa baina yake na Simba.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top