Kikosi cha Rwanda 'Amavubi' kimeanza maandalizi ya mechi yake dhidi ya Tanzania ya kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN2018) nchini Kenya.
Kikosi cha kocha Antoine Hey kitacheza dhidi ya Taifa Stars mwezi ujao. Mechi ya kwanza itachezwa Julai 14 -16 jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana Kigali wiki moja baadaye.
Kipa wa Amavubi, Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye alisema baada ya kupoteza dhidi ya Jamhuri ya Afrika Kati katika kufuzu kwa Afcon 2019, sasa wanatakiwa kujipanga kuivaa Tanzania.
“ Kwa hiyo maandalizi yanahitaji kwa sababu tunahitaji kushindi mechi zote mbili na kujihakikishia kusonga mbele,” alisema huyo Rayon Sports.
Mara ya mwisho Rwanda na Tanzania kukutana ilikuwa katika Mashindano ya Chalenji Cecafa 2015 yaliyofanyika Ethiopia na Amavubi kufungwa 1-2 na Stars katika hatua ya makundi.
Mshindi wa mechi ya Rwanda na Tanzania atacheza na Uganda, inayopewa nafasi kubwa ya kushinda itakapocheza na mshindi kati ya Sudan Kusini na Somalia katika raundi ya pili.
Mashindano ya CHAN yatafanyika Kenya kuanzia Januari 11 hadi Februari 2, 2018.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.