0
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo atapanda kizimbani Julai 31 kujibu mashtaka kutokana na tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili.
Raia huyo wa Ureno anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji kodi inayokadiriwa kufika Pauni 14.7 milioni.
Sakata hilo lilihusishwa na kuondoka mchezaji huyo klabuni hapo, hata hivyo rais wa klabu hiyo amesema Ronaldo ataendelea kuwa mchezaji wao halali.
Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’O mara nne, alidaiwa kunufaika na haki za matangazo ya picha tangu mwaka 2011 na 2014.
Wakati huohuo; Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametuhumiwa kukwepa kodi inayofikia Pauni 3.3 milioni nchini Hispania.
Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi nchini humo imewasilisha malalamiko mahakamani leo Jumanne ikimhusisha raia huyo wa Ureno ambaye amewahi kuifundisha Real Madrid.
Mourinho aliifundisha Real Madrid tangu mwaka 2010 mpaka 2013 na kuiwezesha kutwaa mataji matatu ambayo ni La Liga, Kombe la Mfalme na Supercopa de Espana.
Kocha huyo alirudi Chelsea kabla ya kwenda kukinoa kikosi cha Old Trafford msimu wa 2016/17 huku akifanikiwa kunyakua taji la Europa, Kombe la Ligi.
Uongozi wa Manchester United haujazungumzia lolote kuhusu kocha wake kuhusisha na tuhuma hizo.

Chapisha Maoni

 
Top