Kocha Arsene Wenger amesema bado klabu hiyo inamhitaji Olivier Giroud kuichezea klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao licha ya kutofanya vizuri msimu uliopita.
Giroud alianza mechi 17 pekee katika mashindano yote lakini alifanikisha kupatikana mabao 16.
Tatizo kubwa lililokuwa linamkabiri mchezaji huyo ni majeraha pia bado anakabiliwa na matatizo ya mguu katika kipindi hiki usajili unapoendelea.
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa inasemekana huenda akaondoka kwa mabingwa hao wa Kombe la FA msimu ulioisha na anatajwa kutimkia West Ham.
Hata hivyo, Wenger amejitokeza na kutoa msimamo kwamba bado anamhitaji mchezaji huyo mwenye miaka 30 na umuhimu wake ni mkubwa kikosini hapo.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.