0
Hali ngumu ya kifedha inayoikabili klabu ya Yanga, imeacha pigo baada ya klabu hiyo kushindwa kufika dau kwa kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ambaye sasa anakaribia kutua Simba.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema wameshindwa kuafikiana na Niyonzima kwani fedha alizokuwa akitaja ni nyingi na klabu isingeweza kumpatia.
"Niseme wazi kwamba hatutaweza kuendelea na Niyonzima kwa msimu ujao, tumezungumza ila amehitaji fedha nyingi ambazo klabu imeshindwa kumpatia. Tumemruhusu akatafute maisha mapya," alisema Mkwasa.
Licha ya Mkwasa kufanya siri, tunafahamu kwamba Niyonzima alihitaji Dola 70,000 (Sh 153 milioni) katika mkataba mpya jambo ambalo limeishinda klabu hiyo. Niyonzima huenda akajiunga na Simba hivi karibuni.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top