Mchezaji Tosin Adarabiola amesaini mkataba mpya na Manchester City mpaka mwaka 2021.
Kinda huyo mwenye miaka 19, mkataba wake ulikuwa unaisha mwezi huu na awali kulikuwa na taarifa angeondoka kwenda kutafuta timu mahali kwingine.
Mchezaji huyo ameidhinisha kubaki kwenye dimba la Etihad kwa mkataba wa miaka minne.
Beki huyo wa kati ameitumikia timu ya vijana kwa muda mrefu na alicheza timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza timu hiyo ilipokutana na Chelsea wakati wa mechi ya Kombe la FA mwezi Februari 2016.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.