Afisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amekiri kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Abdulraman Musa anaweza kuondoka timu hiyo na kuwa wamepokea taarifa kutoka kwa timu ndani na nje ya nchi zikitaka sahihi ya mshambuliaji huyo msimu ujao.
Akizungumza Bwire amesema kuwa wanasubiri taarifa kutoka benchi la ufundi kabla ya kufanya maaumuzi yeyote hata hivyo amesema kuwa utaratibu ufuatwe kwa kuwa mchezaji huyo pamoja na kuwa mchezaji wao lakini pia ni muajiriwa wa jeshi.
Ripoti ya Benchi la ufundi
-Ni rasmi ninazo taarifa hizo kwamba vipo vilabu sit u Tanzania lakini nje ya Tanzania tayari zinamuhitaji Abdulraman nitawaomba watanzani kutulia tutatoa taarifa kutokana nayeye mwenyewe ambao wanamuhitaji,nitawaomba watanzania watulie Tutatoa taarifa kutokana nay eye mwenyewe anavyojiskia maamuzi yake binafsi ,tunasubiri taarifa ya mwalimu taarifa ambayo itakuwa ni muongozo wa kutuelekeza tufanye nini .
Aidha Bwire amesema kuwa hawawezi kumkataza kuondoka klabu hiyo lakini akataka taratibu kufuatwa .
Utaratibu kufuatwa
-Sisi ruvu shooting hatumzui mchezaji kuondoka lakini utaratibu ufuatwe Abdulraman ni muajiriwa wa Jeshi,jeshi zina taratibu zake kwa hivyo taratibu hizo zifuatwe sisi kama klabu tutatoa taarifa kutokana na na yeye mwenyewe kwanza anavyojiskia na maamuzi yake.
Hata hivyo Bwire amesema kuwa mchezaji huyo aliweka wazi ndoto yake ya kutaka kuchezea vilabu vya na kuwa asingependa kuvichezea vilabu vya Tanzania.
Ofa za nje ya nchi
-kwa vilabu vya hapa Tanzania Yeye alishatamka kuwa hawezi kwenda kwenda popote ataendelea kuwepo Ruvu Shooting labda hizo ofa zinazokuja akazitafakari na pengine akatoa maamuzi tofauti na hayo y hapo awali”,ameongeza Masau Bwire.
Abdulrahman ambaye alikuwa mfungaji bora wa ligi Kuu Tanzania bara akiwa amewafungia Ruvu Shooting mabao 14 sawa na sImonMsuva wa Timu ya Yanga amekuwa kivutio cha timu nyingi huku wengi wakiendelea kuwinda saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.
Chapisha Maoni