0
Michuano ya Sportspesa Super Cup inatarajiwa Kuanza rasmi Jumatatu ambapo Timu 8 nne za Tanzania na nne za Kenya zinatarajiwa kucheza katika mashindano hayo ambayo yatafanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam.
Kocha Mkuu wa AFC Leopards ya kutoka nchini Kenya Dorian Marian, ameahidi kuwa watafanya vizuri katika michuano hiyo ili kurejesha hadhi ya timu hiyo katika mashindano ya kimataifa.
-Hakuna njia nyingine bora ya
AFC Leopards kuwashukuru mashabiki wake Ila tu kwa kushinda na kuleta ubingwa nyumbani ",amesema kocha huyo mromania ambaye amejiunga na timu hiyo mapema mwezi huu.
AFC Leopards ambao hawajafanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Kenya wakimaliza katika nafasi ya 12 wakiwa na alama 15, watafungua michuano hiyo kwa kupambana dhidi Singida United, waliopanda Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Mabingwa wa Tanzania na Kenya
Wakati huohuo Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya Tusker FC wameahidi kuendeleza ubabe wao pale watakapokutana na Mabingwa wa Ligi Kuu soka nchini Tanzania, Yanga SC katika mchezo wa pili utakaoanza majira ya saa 10:30 Jioni.
Akizungumza kuhusu Mechi hiyo Nahodha wa Tusker Fc James Situma amesema kuwa michuano hiyo ni muhimu kwao kwa kuwa itawapa uzoevu wa kimataifa.
Uzoevu
-Mashindano haya yatatusaidia kupata uzoevu wa kimataifa ambao utaisaidia katika jitihada zetu za kufanya vizuri kimatifa",amesema Situma.
Timu zingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni Gor Mahia watakaocheza dhidi ya Jang'ombe Boys ya Zanzibar nao Nakuru All Stars inayoshiriki Ligi daraja la pili ikicheza dhidi ya Mabingwa wa Azam Sports Federation Cup Simba Sc, ikiwa ni michezo itakayofanyika siku ya Jumanne.
Everton
Mshindi katika michuano hiyo pamoja na kupewa zawadi ya zaidi ya shilingi milioni 60 atacheza dhidi ya Timu ya Everton FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini England.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top