Mshambuliaji wa Arsenal, Yaya Sanogo ametupwa nje kwenye usajili wa msimu 2017/18 kutokana na kufanya vibaya msimu ulioisha.
Sanogo alijiunga na Arsenal mwaka 2013 akitokea Auxerre. Amecheza mechi 20 katika mashindano yote akiwa dimba la Emirates, huku akifunga bao moja tu.
Suala la kutolewa kwa mkopo kwenda Crystall Palace, Ajax na Charlton Athletic bado halijathibitishwa.
Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika Juni 30.
Wachezaji wengine walioonyesha mlango wa kutokea ni Stefan O’Connor, Kristopher da Graca pamoja na Kostas Pileas wote wakiwa wanacheza timu ya vijana ya klabu hiyo.
Chapisha Maoni