Mwanza. Kipa wa Mbao FC, Benedict Haule amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote itakayompa dau nono.
Kipa huyo aliisaidia Mbao kubaki katika Ligi Kuu pamoja na kucheza mechi ya nusu na fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga na Simba.
Haule alisema yupo tayari kufanya kazi katika timu yoyote itakayomsajili kwa dau zuri kwa kuwa soka ndiyo maisha yake yalipo.
Kipa huyo alisema Majimaji na Mbao FC zimeshafanya mazungumza naye, lakini bado hawajafikia muafaka na kwamba atakayewahi ndiye atapata saini yake.
Alikanusha taarifa ya kutakiwa na Singida United akisema hizo ni tetesi za mitaani, lakini bado hajakutana na viongozi wa timu hiyo.
Chapisha Maoni