Mchezaji wa zamani wa Yanga, Majimaji na AFC Arusha, Allan Shomari ameshangazwa na tabia ya Simba na Yanga kugombania saini za wachezaji katika dirisha hili la usajili.
Mkongwe huyo anayesumbuliwa na tatizo la kutoona anasema kitendo kinachofanywa na viongozi wa Simba na Yanga ni dhahili wameshindwa kutafuta wachezaji wengine.
“Haiwezekani kila mwaka unasikia timu hizi mbili zinagombania wachezaji ambao viwango vyao siyo vya kutisha ukilinganisha na wachezaji waliopo na wanaotumikia timu zao tatizo lililopo bado hawajaonyesha kuwaamini na kuwapa muda wachezaji wazawa.”
“Kila siku nasikia Okwi mara Niyonzima inamaana hawajaona wachezaji wengine ambao wengeleta sura mpya katika soka la Tanzania na kuongeza ushindani kwa wazawa waliopo?”alihoji Shomari.
“Timu zetu zingekuwa na utaratibu wa kuwa na academy zao kama ilivyo kuwa kwa timu ya Azam Fc kwa kukuza wachezaji toka chini wasingepata tatizo la kugombania wachezaji na ingekuwa msaada mkubwa hata kwa Taifa katika kuiunda Taifa Stars”
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.