0
Timu ya Soka ya Yanga ambao ni mabingwa wa soka Tanzania Bara wamefanikiwa kutinga katika hatua ya Nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwatoa Mabingwa wa Kenya Tusker Fc kwa jumla ya penati 4-2 baada ya Dakika 90 kumalizika Kwa Sare ya 0-0.
Mchezo huo ulikuwa wa kiufundi kwa kila upande huku Yanga wakiingia wakiwa na Sehemu kubwa ya Vijana wa Timu B kama Mohamed Ally, Yusufu Mhilu, Maka Edward huku wachezaji nyota wakiwa ni Mlinda mlango Deogratius Munish, Obrey Chirwa, Nadir Haroub pamoja na Juma Abdul.
Dakika 90.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kulisakama lango la
Tusker FC kwani dakika ya 8, kiungo wa Kati Juma Mahadhi alipiga Shuti kali ambalo liligonga Mwamba wa Juu kabla ya Kutoka nje.
Azikupita dakika nyingi sana kwani katika dakika ya 14 Mwakalukwa aligongewa pasi murua na Kiungo Juma Mahadhi lakini kukosekana kwa umakini kukamfanya kushindwa kuunganisha pasi hiyo na mpira uliambaa ambaa na kutoka nje.
Katika dakika ya 19 almanusura Tusker FC wapate bao kufuatia makosa ya Yusuph Mhilu ambaye aliurudisha mpira nyuma kwa kipa Deogratius Munish ambapo ulimkuta Mshambuliaji wa Tusker Fc ambaye naye hakuwa makini na kushindwa kuandika Bao.
Hadi filimbi ya Mwisho Yanga Bila Tusker Bila, hivyo yakaamuliwa matuta kupigwa ili kumpata mshindi wa mchezo huo ambapo Yanga wakafanikiwa kupata Penati 4 huku Tusker FC wakiambulia Penati 2.
Nusu fainali.
Kwa ushindi huo sasa Yanga watakutana na AFC Leopards katika hatua ya Nusu fainali itakayopigwa Juni 8 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Aidha Michuano hiyo itaendelea Kesho Jumanne kwa michezo miwili ambapo Mchezo wa Mapema Jang'ombe Boys watacheza na Mabingwa wa Zamani wa Kenya, Gor Mahia Huku Simba SC wakikutana na timu ya Ligi daraja la Pili, All Stars ya Kenya.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top