0
Timu ya AFC Leopards kutoka Kenya imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Sportspesa Super Cup inayoshirikisha Timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambayo imeanza kwa kishindo mchana huu katika mchezo wa ufunguzi ambao umefanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
AFC Leopards ambao wameibuka na ushindi wa 5-4 kupitia mikwaju ya penati baada ya mchezo huo kukamilika kwa sare ya 1-1 na hivyo hukumu ya matuta kulazimika kutumika ili kumpata mshindi aytakaye songa hatua ya Nusu Fainali.
Historia
Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa nane mchane umeshuhudia Singida United wakiandika historia ya kuwa timu ya kwanza kupata bao baada ya kiungo mzimbabwe Kutinyu kufunga bao la kichwa mnamo dakika ya 13 kwa kuunganisha kwa kichwa kona ya Salumu Chuku.
Kipindi cha pili AFC Leopards walianza kwa kasi huku kocha akifanya mabadiliko ambayo yalionekana kuzaa matunda katika dakika ya 63 AFC Leopards wakapata bao la kusawazisha baada ya Mghana Gilbert Fiamenyo kufunga bao safi .
Nafasi za wazi
AFC Leopards ambao walipata nafasi nyingi za wazi wakifunga mabao mawili ya kuotea ambayo yalikataliwa na muamuzi wa mchezo huo.
Kufuatia ushindi huo AFC Leopards wanafuzu hatua inayofuta .
Aidha mchezo wa pili ni utawakutanisha Bingwa wa Tanzania Yanga SC dhidi ya Bingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya .

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top