Wakala wa Donnarumma, Mino Raiola amesisitiza kuwa bado hawajafanya mazungumzo na klabu yoyote lakini kipa huyo wa Kiitaliano yupo tayari kutua Madrid
Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma yupo tayari kutimkia Real Madrid kwa mujibu wa wakala wake, Mino Raiola.
Donnarumma amekuwa kipa mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kucheza Serie A akiwa na umri wa miaka 16 tu, tangu alipokuwa mlinda mlango nambari moja wa Milan licha ya kutimiza miaka 18 Februari.
Kinda huyo, mwenye kimo cha futi 6 na nchi 5 pia amekuwa kipa mdogo zaidi kuichezea timu ya taifa ya Italia Septemba mwaka jana mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa.
Donnarumma amekataa mkataba mpya San Siro, ikimaainisha atakuwa akipatikana kama mchezaji huru majira ya joto iwapo Milan watakataa kumuuza kuelekea kampeni za 2017-18.
Raiola amekanusha habari kuwa amefanya mazungumzo na klabu yoyote, lakini wakala huyo amesisitiza kuwa mteja wake yupo tayari kucheza Real Madrid.
"Ofa kutoka kwenye timu nyingine? Timu zinazozungumziwa ni zile zilizokuwa zikimfuatilia tangu akiwa na umri wa miaka 14, kwa hiyo kama alitaka kuondoka angeshafanya hivyo siku nyingi. Hatujafikia makubaliano na timu yoyote. Je! Donnarumma yupo tayari kucheza Real Madrid? Naam tangu kuzaliwa kwake alikuwa tayari," Raiola aliwaambia waandishi.
Donnarumma kwa sasa yupo na timu ya Italia umri chini ya miaka 21 kwenye michuano ya Ulaya chini ya miaka 21 Poland.
Chapisha Maoni