TIMU ya taifa ya Vijana U17 ya Sudan Kusini, mchana wa jana Jumapili walianza vema mbio zao za kusaka tiketi ya kucheza fainali za AFCON kwa Vijana za mwaka 2019 baada ya kuwafumua majirani zao, Djibouti kwa mabao 2-1.
Ushindi huo umeiweka Sudan Kusini kileleni mwa kundi B (kabla ya matokeo ya mechi ya jioni ya jana kati ya Uganda na Ethiopia).
Mabao ya washindi hao yaliwekwa kimiani na Deng Joseph katika dakika ya tano na Victor Charles dakika ya 26 kabla ya Djibouti kupata la kufutia machozi dakika ya 64 kupitia Remi Ahmed.
Michuano hityo itaendelea tena jioni ya leo Jumatatu kwa mchezo mmoja tu kati ya Burundi na Rwanda.
Chapisha Maoni