Winga wa Chelsea Willian anasema kuwa hakuna sababu ambayo ingemfanya kusalia katika klabu hiyo iwapo aliyekuwa mkufunzi wa klabu hiyo Antonio Conte angeendelea kuwa mkufunzi.
Conte alishinda taji la ligi ya Uingereza 2016-17 lakini akafutwa mwezi Julai baada ya kumaliza katika nafasi ya tano.
Mrithi wake aliyekuwa mkufunzi wa Itali Maurizo Sarr alishinda mechi yake ya kwanza ya ligi baada ya kuilaza Huddersfiedl 3-0 siku ya Jumamosi.
''Meneja anatuambia tucheze tujifurahishe uwanjani'' , Williana alisema. ''Ni raha kucheza hivi , nadhania hivyo''.
''Tuna wachezaji wengi walio na ubora mbele kama vile Eden Hazard na Pedro. Wachezaji kama hao wanataka kucheza. Ndio maana yeye Sarri anataka tucheza mchezo mzuri baada ya kuwasili Cheslea''.
''Hivi ndivyo tutakavyoweza kucheza msimu huu''.
Raia huyo wa Brazil , 30, alikuwa akihusishwa na Barcelona, Real Madrid na Manchester United msimu huu lakini akaamua kusalia na The Blues mapema Agosti.
Alipoulizwa iwapo angesalia kama Conte angeendelea kuwa mkufunzi , aliambia jarida la Evening Standard, ''hakuna sababu hakiuna''.
''Niko hapa kwa sababu nataka kucheza kandanda'',.
''Nitaondoka iwapo Chelsea inataka niondoke''.
Chelsea itakaribishwa na Arsenal nyumbani katika mechi yao ya pili siku ya Jumamosi ijayo, na Willian ameongezea: sasa tuna mbinu mpya ndio maana tunaweza kuiletea matatizo Arsenal.
''Kwa kweli itakuwa mechi spesheli dhidi ya Arsenal kwa sababu ni debi .Huwa mechi ngumu dhidi yao .Ni lazima tujiandae vyema wiki hii''.
Chapisha Maoni