0
Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kupitia bodi ya Ligi limepangua ratiba ya mechi za awali za Ligi kuu Tanzania bara kwa vilabu vya Simba na Yanga kutokana na kupokea barua kutoka serikalini kuhusiana na matumizi ya uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa bodi ya Ligi Boniface Wambura amethibitisha kuwa wamepokea barua hiyo inayosema uwanja huo hautotumika kuanzia Agosti 23 hadi 30.
Wambura amesema mechi tatu za Simba Sc dhidi ya Tz Prisons, Lipuli Fc na Mbeya City zote zimehamishiwa uwanja wa uhuru na ule wa Yanga Sc uliopangwa kuchezwa Agosti 23 katika dimba la Jamhuri Morogoro utapigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam huku Yanga Sc akiwa mwenyeji

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top