Kazi kweli: Mbunge wa Nkasi mh. Ally Kessy asema Wazanzibar Wanachosha, ni Mzigo
Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara ya
mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge
wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha
matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu
wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu
kuwa wanabaguliwa , wanadai mambo mengi
kuliko uwezo wao na wakati hawachangii hata
senti kwenye Muungano na hivyo kama
wanaona wanaonewa waende kwenye nchi yao
sio kukaa kwetu.......
Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar
Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba
ukipigania filimbi wananchi wote
wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za
mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki , na
pia hata umeme hawalipi na maji pia .
jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu
Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka
naibu Spika a mwambie Kessy kamwe
asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa baada ya
kumuita mwendawazimu , na alisema ni bahati
mbaya kwa CCM kuwa na mbunge
mwendawazimu kama huyu ......
Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka ,
sijui nini maana yake .."...
Chapisha Maoni