0
 Hitmaker wa ‘Anita’ Matonya aliwekewa vitu vinavyohisiwa kuwa ni madawa kwenye pombe aliyokuwa akinywa, kwa mujibu wa Rich One ambaye ni jirani yake.

Picha ya Matonya inayomuonesha akiwa amelala vichakani hajitambui ilisambaa wiki hii kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha watu kuzusha kuwa amefariki dunia.
Rich alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa tangu afahamiane na Matonya hajawahi kumuona amekunywa pombe hadi kufikia hatua ya kupoteza.
"Nina imani kuwa washkaji waliokuwa naye walimwekea,” alisema rapper huyo. Bado Matonya hajaweza kuzungumzia skendo hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top