KLABU ya Manchester United imekubali kuingia Mkataba wa miezi 18 na kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes.
Klabu hiyo inajiandaa kumtangaza rasmi kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 kusajiliwa kwake Old Trafford akasaidiane na David de Gea.
Valdes amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Louis van Gaal kwa miezi miwili iliyopita akiwa mchezaji huru aliyetoka kupona majeruhi.
Valdes amepona maumivu ya goti
yaliyomuweka nje ya Uwanja tangu Machi mwaka jana

Kocha wa United, Louis van Gaal hajazungumza mengi juu ya mipango yake kwa Valdes, lakini amevutiwa naye kiasi cha kutosha siku za karibuni kiasi cha kuridhia kumpa mkataba.
Kuwasili kwa Valdes kutamoa De Gea ushindani wa kutosha Old Trafford kwa mara ya kwanza.
Kipa wa pili kwa sasa, Anders Lindegaard hana nafasi mbele ya Van Gaal.
Chapisha Maoni