0
TIMU ya Real Madrid imefungwa mabao 2-0 na wenyeji Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey Uwanja wa Vicente Calderon usiku huu.

Mshambuliaji Fernando Torres aliichezea kwa mara ya kwanza klabu yake ya zamani, Atletico baada ya kurejea wakati Cristiano Ronaldo alikuwa nje kwa maumivu ya goti.
Winga Gareth Bale aliifungia bao Real mapema, lakini likakataliwa kwa sababu alikuwa ameotea, kabla ya Raul Garcia kuifungia bao la kwanza Atletico dakika ya 58 kwa mkwaju wa penalti
kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa na Sergio Ramos.

Jose Gimenez akamfurahisha zaidi kocha wake Diego Simeone kwa kufunga bao la pili dakika ya 76. Mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Bernabeu Alhamisi ya Januari 15 na Real wanatakiwa kushinda 3-0 ili kutinga Robo Fainali.
 Mshambuliaji wa Atletico, Fernando Torres (kushoto) akikimbia na mfungaji wa bao lao la kwanza, Raul Garcia (kulia) kushangilia

Chapisha Maoni

 
Top