News: Jeshi la Nigeria Limebaini Walikofichwa Wasichana Waliotekwa
Jeshi la nchini Nigeria limesema linajua mahali
walikofichwa zaidi ya wasichana 200
waliotekwa wakiwa shuleni lakini hawawezi
kuitaja sehemu hiyo hadharani.
Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la
Boko Haram ambalo linadai haliwezi
kuwaachia hadi watakapobadilishana
wafungwa wao na serikali ya nchi hiyo. Kwenye kituo cha TV cha Nigeria, imetangazwa
kwamba japo imefahamika walipo Wasichana
hao ambao bado wanashikiliwa mateka…..
majeshi ya Nigeria na mengine yanayoendesha
opareshen hiyo hayatotumia nguvu za kijeshi
kwenye uokoaji wa wasichana hawa.
Kitendo cha kutekwa kwa wasichana hao
kimeibua majonzi makubwa miongoni mwa
wazazi na kufanya kuibuka kwa kampeni
iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na
vyombo vya habari yenye jina la Bring Back
Our Girls ikimaanisha “Rudisheni wasichana
wetu”
Chapisha Maoni