Jeshi la polisi lapiga marufuku Vigodoro Dar es Salaam
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es
salaam limepiga marufuku ngoma za
kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika
nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali
Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa
kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo
yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu
kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo
wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo
kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda
wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam
Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa
ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za
usiku’ Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni
inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya
kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia
wafuasi zaidi ya mia moja ambapo pia watu
wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu
vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa
ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja
‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo
kali kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia
sasa.
Chapisha Maoni