News: Mama mzazi wa Zitto Kabwe afariki dunia
Rais Jakaya Kikwete alipomjulia hali Mama
Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa
tiketi ya CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe
aliyekuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa
wenye kuhitaji uangilizi maalumu (ICU) katika
hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam hivi
majuzi. (picha: Freddy Maro/IKULU)
**********
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum,
ambaue alikuwa mama mzazi wa Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA, aliyekuwa amelazwa
katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya
Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na
maradhi ya saratani, amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari
mbalimbali, bi. Shida alianza kusumbuliwa na
maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka
jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka
huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa
pamoja na wajumbe wengine wa Bunge
Maalumu la Katiba.
Zitto alinukuliwa akisema kuwa, baada ya hali
ya mama yake kuwa mbaya alishindwa
kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa
na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa
na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa
tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa
India kwa matibabu zaidi. Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo,
alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa
nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.
Zitto, ingawaje alisema hali ya mama yake
haikutengemaa tangu aanze kusumbuliwa na
maradhi hayo, alikuwa na matumaini: “Hali ya
mama kwa kweli siyo nzuri, lakini nina imani
itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za
ujenzi wa taifa kama zamani,” alisema Kabwe
ambaye alidai kuwa kutokana na maradhi hayo
ya mama yake, alishindwa kuhudhuria Bunge
la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto
alionekana Dodoma mara moja tu, siku
ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Viongozi na wasanii mbalimbali wametuma
salamu za pole kwa Zitto Kabwe.
Bernard Membe
Zitto kabwe pole sana kwako na ndugu kwa
Msiba huu mzito. Tunawaombea subira na
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala
pema peponi..Amina
William Ngeleja
Nimepokea Taarifa za msiba wa Bibi Shida
Salum(mama mzazi wa Mhe. Zitto Kabwe) kwa
masikitiko makubwa. Nawapa pole familia
nzima ya ndugu yetu Zitto katika kipindi hiki
cha Majonzi. Mwenyezi Mungu awape Wepesi ,
na Pia natoa pole kwa wote walioguswa na
Msiba wa George Otieno aliyefariki Jana.
Tuendelee kuziombea familia hizi na zingine
zenye misiba ili wapate faraja kutoka kwa
Mwenyezi Mungu ambaye ni mfariji Mkuu!
Jokate Mwegelo
Zittokabwe I’m so so sorry Zitto. May her soul
rest in peace. Amen!!
Linex Sunday
Nachukua nafasi hii kuipa pole familia ya Zitto
Ruyagwa Kabwe Ndugu jamaa Marafiki kwa
kumpoteza Bi Shida Mungu awape nguvu
katika kipindi hichi kigumu R.I.P Bi shida
tulikupenda lakini Yeye aliyekuleta
amekupenda zaidi Jina LA Bwana libalikiwe na
mapenzi yake yatimie.
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter,Zitto
Kabwe ameandika:
Chapisha Maoni