CUF kimelaani vikali kitendo cha kupigwa na kudhalilishwa kwa wanahabari nje ya makao makuu ya polisi wakati wakifwatilia sakata la kuitwa mh MBOWE mwishoni mwa wiki jana.
Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza kuunga mkono harakati zinazofanywa na chama cha democrasia na maendeleo
CHADEMA za kuandaa maandamano
nchi nzima kupinga kuendelea kwa
bunge maalum la katiba na kusema
kuwa chadema kipo sawa na
maandamano hayo ni halali na watatoa
ushirikiano wote katika maandamano
hayo.
Akizungumza jumapili hii na wanahabari
jijini Dar es salaam mwenyekiti wa
chama hicho Profesa IBRAHIMU
LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA
kama chama cha siasa ni jukumu na ni
haki yao kufanya maandamano pale
ambapo wataona kuna ubadhilifu wa
fedha za wananchi unatokea katika nchi.
Aidha LIPUMBA akizungumzia sakata la
kuitwa na kuhojiwa kwa mwenyekiti wa
CHADEMA na kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni Mh FREMAN MBOWE
amesema kuwa hakuna sababu yoyote ya
msingi ya kumhoji kiongozi huyo kwani
maandamano yote yanayoitishwa na
CHADEMA yanafwata taratibu zote ila
kinachotokea ni polisi kutokujua sheria
za maandamano. Na kusema kumwita
Mh. Mbowe ni kumdhalilisha kiongozi
huyo mkubwa wa upinzani wakati
anatekeleza haki yake ya kikatiba.
“kazi ya polisi sio kuruhusu maandamano
ya chama chochote, sisi tunatoa taarifa tu
kwa polisi ili watulinde,na hatuombi kibali
cha polisi kiufanya kibali, polisi
wanadhani kuwa sisi tunaomba kibali cha
maandamano wakati ni haki ya kikatiba
kabisa ya kuandamana na kufanya
mikutano ya adhara".
Mh LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA
sio chama cha kwanza kutangaza
maandamano ya nchi nzima kuhusu
jambo la katiba kwani mapema baada ya
hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati
anafungua bunge la katiba chama cha
mapinduzi nao walitangaza mikutano na
maandamano nchi nzima ambayo
hayakupingwa na polisi ila anashangaa
upinzani kunyimwa haki hiyo ya msingi.
Chapisha Maoni