0
MANCHESTER United imechapwa mabao 5-3 na Leicester City ugenini jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, mshambuliaji Radamel Falcao akianza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu kwa mkopo kutoka Monaco.

Robin van Persie aliifungia United bao la
kuongoza dakika ya 13 akiunganisha krosi ya Falcao kabla ya Angel di Maria kufunga la pili dakika tatu
baadaye.

Leonardo Ulloa akaifungia Leicester bao la kwanza kabla ya Ander Herrera kuifungia la tatu United.
David Nugent akaifungia bao la pili Leicester kwa penalti ya utata iliyotolewa dhidi ya
Rafael na Esteban Cambiasso akafunga la tatu dakika ya 63.

‘Kifo’ cha Man United leo inayofundishwa na Mholanzi, Louis Van Gaal aliyetumia Pauni
Milioni 150 kusajili kilikamilishwa na Jamie Vardy aliyeifungia bao la nne Leicester zikiwa zimebaki dakika 12 na Ulloa aliyefunga la tano kwa penalti iliyosababishwa na Tyler
Blackett ambaye alitolewa nje kwa adi
nyekundu.

Kikosi cha Leicester kilikuwa: Schmeichel, De Laet, Morgan, Moore, Konchesky, Hammond, Drinkwater, Cambiasso/King, Nugent/James,
Ulloa nja Vardy/Schlupp.

Man Utd: De Gea, Da Silva, Evans/Smalling, Blackett, Rojo, Blind, Ander Herrera, Di Maria/ Mata, Rooney, Falcao/Januzaj na Van Persie.

Chapisha Maoni

 
Top