MANCHESTER United imejitutumua na kupata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Old Trafford, licha ya kucheza pungufu baada ya Nahodha wake, Wayne Rooney kutolewa kwa kadi
nyekundu.
Rooney alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 60 baada ya kumkwatua kwa nyuma kiungo wa West Ham, Stewart Downing.
Lakini Rooney aliondoka uwanjani akiwa
tayari ameifungia United bao lililokuwa la kwanza dakika ya tano, kabla ya Robin van Persie kufunga la pili dakika ya 23.Makosa ya kipa wa United, David De Gea
yaliipa Hammers bao la kufutia machozi
lililofungwa na Diafra Sakho dakika ya 37. Kevin Nolan aliifungia West Ham bao ambalo lingekuwa la kusawazisha dakika ya mwisho, lakini bahati alikuwa amekwishaotea.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Rafael, McNair, Rojo, Shaw, Blind, Herrera/Valencia dk74, Di Maria/Thorpe dk90, Rooney, Van Persie na Falcao/Fletcher dk65.
West Ham: Adrian, Demel/Jenkinson dk65, Tomkins, Reid, Cresswell, Song, Poyet, Amalfitano/Cole dk61, Downing, Sakho na E Valencia.
Chapisha Maoni