0
Msanii wa kitambo wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na Kundi la Chamber Squad na ngoma yake ya taifa ya Kama Vipi, Moses Bushagama
‘Mez B’ anadaiwa kuwaaibisha ma-miss kwa kuwalazimisha kupiga nao picha wakiwa watupu.

Tukio hilo la kidhalilishaji na lisilovumilika lilijiri juzikati kwenye Ufukwe wa Mikadi uliopo Kigamboni jijini Dar muda mfupi baada ya jamaa
huyo ‘kushuti’ video ya ngoma yake mpya ya Shemeji.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, jamaa huyo aliwafuata warembo hao waliojitambulisha kwa majina ya Vicky na Rebecca waliokuwa kwenye
swimming pool (bwawa la kuogelea) ambao ilisemekana kuwa siyo raia wa Bongo na huko wanakotokea ni ma-miss.

Ilidaiwa kwamba Mez B ndiye aliyewaomba kupiga nao picha lakini jamaa huyo ‘akaharibu’ baada ya
kwenda mbele zaidi na kuanza kuwaminya ‘vifuu’ vyao kifuani vilivyoonekana ni vya saa sita
vilivyokuwa wazi bila hata ‘braa’.
Ilisemekana kwamba baada ya kupiga picha hizo, yeye (Mez B) aliwafowadia washikaji zake ndipo zikazagaa kupitia mtandao wa WhatsApp.

Kumekuwa na kasumba ya kupiga picha za utupu kisha kuziachia mtandaoni kwa kudhani kuwa ni kujiongezea umaarufu lakini ukweli ni kujiondolea utu na heshima mbele ya jamii.

Chapisha Maoni

 
Top