Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro, kimepanga kufanya mapokezi ya wajumbe waliokuwa katika Bunge la Katiba wakiwawakilisha
wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mapokezi hayo, yanatarajiwa kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kuelekea ofisi za CCM mkoa, na kufuatiwa na
mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi mjini Moshi.
Akizungumzia maandalizi hayo, Katibu wa CCM mkoani hapa, Deogratius Ruta, alisema kuwa wanachama wa CCM na wananchi wengine, wameamua kufanya mapokezi hayo baada ya wajumbe hao kufanikiwa kupitisha Rasimu ya
Katiba.
Wajumbe waliokuwa kwenye Bunge hilo kutoka mkoani Kilimanjaro ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe, Mbunge wa Jimbo la Siha, Agrey Mwanri, Mbunge wa
Jimbo la Moshi- Vijijini Dk. Ciril Chami.
Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Same-
Magharibi, David Mathayo, Mbunge wa Jimbo la Same- Mashariki, Anna Kilango Malechela, na Mbunge kutoka Vunjo, Dk. Agustino Lyatonga Mrema.
Wajumbe wengine wawili wa kuteuliwa na Rais ni Wanasheria, Elizabeth Minde na Evodi Mmanda.
Chapisha Maoni