0
MSHAMBULIAJI Edinson Cavani jana alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioonyeshwa kadi nyekundu wakati Paris St Germain ikiitandika RC Lens mabao 3-1 katika mchezo wa Ligue 1 Uwanja wa Stade de
France.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipewa kadi hiyo na refa Nicolas Rainville, baada ya kushangilia bao la mwisho la timu yake kwa ishara ya kupiga bunduki, staili maarufu kwa klabu ya Arsenal ya England.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameponda maamuzi hayo ya utata akisema kwamba kama adhabu zitatolewa kwa ushangiliaji wa
aina hiyo, ni mbaya kwa soka ya Ufaransa.

Mabao ya PSG yalifungwa na Cabaye dakika ya 28, Maxwell dakika ya 33 na Cavani dakika ya 55, wakati Lens pia ilipoteza wachezaji wawili waliotelewa kwa kadi nyekundu, Gbamin na Le Moigne, huku bao lao la kufutia machozi likifungwa ma Coulibaly dakika ya
10.

Chapisha Maoni

 
Top