nje kidogo ya Mji wa Bukoba na kumkata mguu mtu mwingine wakati wakifanya maombi kanisani.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa wakati mwalimu huyo pamoja na mwenzake aliyetambuliwa kwa jina moja la Themistocles ambao ni waumini wa Kanisa la Pentecostal Asemblies of God (PAG) walipoamua kuendelea na
mkesha baada ya wenzao kuondoka.
Kwa mujibu wa Mchungaji wa kanisa hilo, Faustin Joseph saa chache kabla ya mauaji hayo walikuwa wakifanya maombi wakiwa kundi la watu
wanne na ilipofika saa tano usiku waliondoka na kuwaacha wenzao wawili.
‘’Tunao utaratibu wa kufanya maombi, ilipofika saa tano usiku mimi na mwenzangu mmoja tuliondoka na kuwaacha wenzetu wawili na
ilipofika saa nane usiku nilipigiwa simu na majirani kuwa kuna mauaji yamefanyika kanisani,’’ alisema mchungaji huyo.
Pia, mchungaji huyo alibainisha kuwa wauaji hao hawakuchukua mali yoyote na kuwa siku chache kabla ya mauaji hayo watu wasiojulikana
walivamia kanisani hapo na kuiba viti pamoja na vitambaa jambo alilosema liliwafanya waone umuhimu wa kuchukua tahadhari.
Akizungumzia mauaji hayo Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste mkoani Kagera, Crorwad Edward alisema tukio hilo limewaletea mshtuko na kuwa wanajiandaa kutoa tamko kwa
kuwa pia yaliwahi kuwepo matukio ya kuchoma moto makanisa.
Akithibitisha kuwapo kwa mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema muumini huyo ni Mwalimu wa Sekondari
ya Kagemu na kuwa majeruhi aliyekatwa mguu amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Pia, alisema kuwa tayari wameanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo aliyosema yamefanywa na watu wanne na kuwa mtuhumiwa mmoja
amekamatwa kwa ajili ya mahojiano na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Chapisha Maoni