waandamanaji kuwa ajiuzulu na badala yake ametoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo wakubali mabadiliko ya kisiasa yaliyopendekezwa na Serikali
Kuu ya Uchina.
Sheria hizo zilizotangazwa mwisho wa Agosti, zimezusha maandamano ya maelfu ya watu katika eneo hilo lililokuwa wakati mmoja koloni ya
Uingereza.
Akizungumza katika sherehe ya kitaifa ya Uchina, Mkuu wa Hong Kong, CY Leung, alisema kuwa kila mtu atakuwa na fursa ya kumpigia kura kiongozi
katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanywa baada ya miaka mitatu, iwapo jiji hilo la Hong Kong litakubali kuidhinisha mabadiliko ya uchaguzi
kama ilivyopendekezwa na Serikali Kuu ya Uchina.
Lakini maafisa wa Uchina wamesema kuwa ni wagombeaji ambao wanawaamini pekee ndio watakaopata fursa ya kuwania viti mwaka wa 2017.
Wazo hilo limekataliwa na makumi ya maelfu ya waandamanaji ambao sasa wamekalia barabara zote za Hong Kong wakitaka mamlaka kuamua ni
nani anayestahili kugombea viti katika uchaguzi.
Chapisha Maoni