Marubani wa ndege za kivita za Iraqi zilizokuwa na maji, vyakula na misaada mingine ya kibinadamu zimesambaza mahitaji hayo kwa maadui zao wa kundi la Islamic States badala ya
kuwapa wanajeshi wao.
Kwa mujibu wa NBC mmoja kati ya wabunge wa Iraqi ambaye pia ni afisa wa ngazi za juu za usalama, Hakim Al-Zamili ameeleza kuwa
kutokuwa na uzoefu wa kutosha kwa marubani hao kumewafanya wadondoshe misaada hiyo
katika eneo linalodhibitiwa na kundi la ISIS badala ya eneo walilokuwapo wanajeshi wao ambao walikuwa wakihitaji sana msaada huo.
“Wale wanajeshi walikuwa wanahitaji sana misaada ile, lakini kwa sababu ya mipango isiyo sahihi ya makamanda wa jeshi la Iraqi na ukosefu
wa uzoefu wa marubani, tuliwasaidia wapiganaji wa ISIS kuwaua wanajeshi wetu.” Al-ZAMILI ameiambia NBC.
Marekani na washirika wake wameendelea kulisaidia jeshi la Iraqi huku wakiendesha mashambuzi ya anga dhidi ya kundi la ISIS lilishikilia maeneo kadhaa nchini Syria na Iraqi.
Chapisha Maoni