0
HALMASHAURI Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomaliza kikao chake jana jioni Mjini Dodoma, imeunga mkono katiba iliyopendekezwa kwa asilimia 100.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema
Bunge Maalumu la Katiba lilifanya kazi nzuri ambayo inastahili kupongezwa.
Kutokana na hilo, alisema NEC inaunga mkono Katiba Inayopendekezwa kwa asilimia 100 na kupongeza kazi nzuri iliyofanywa na Bunge Maalumu la Katiba.

“Halmashauri Kuu chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete imeridhia kazi iliyofanywa na Bunge maalum la katiba,” alisema.
Alisema halmashauri kuu inawaomba wananchi kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini mkubwa na kuielewa ili wakati ukifika waweze
kuipigia kura ya ndiyo.
Pia alisema halmashauri hiyo imepitisha kanuni za Shirikisho la vyuo vikuu nchini, kwani awali licha ya kuanzisha mikoa ya vyuo vikuu kichama,vlakini kulikuwa hakuna kanuni za kuendesha
mikoa hiyo.

Akizungumzia suala la uchumi kwenye chama alisema halmashauri hiyo imepitisha sera maalumu ya kujitegemea kwenye chama katika
ngazi zote. Alisema lengo ni kuondokana na utegemezi katika kuendesha kazi za chama kwa kutumia ruzuku.

Chapisha Maoni

 
Top