SIMBA SC imetoa sare ya tano mfululizo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Prisons jioni hii Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
Simba SC ilikaribia kabisa kuondoka na
ushindi katika mchezo huo, lakini makosa yaliyotokana na uzoefu mdogo wa kipa Peter Manyika, yaliizawadia bao jepesi la kusawazisha Prisons dakika ya 89.
Manyika alianguka akalala kwenye boksi, refa akamuambia inuka- wakati huo mchezo unaendelea, naye akainuka na wakati anarudi kangoni, Hamisi Maingo akapiga shuti langoni
la kufunga.Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya nane kwa shuti la mpira wa adhabu, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Jumanne Elfadhil.dk78 kipind
cha pili pas javu Simba SC inaokota pointi ya tano katika mechi tano na sasa inaelekea katika mchezo
mwingine wa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar wiki ijayo.
Kikosi cha Prisons kilikuwa; Mohammed
Yussuf, Salum Kimenya, Laurian Mpalile,
Lugano Mwangama, James Mwasote,
Jumanne Elfadhil, Jeremiah Juma, Freddy Chudu, Ibrahim Hassan, Amir Omar na Lambert Sabianka.
Simba SC; Peter Manyika, William Lucian
‘Gallas’, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,
Hassan Isihaka, Joseph Owino, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla/ Amri Kiemba dk58, Elius Maguli, Amisi Tambwe na Emmanuel Okwi.
Chapisha Maoni