Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwadui uliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wa jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd
Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung’olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia
kombeo (kwa lugha ya kisukuma Nh'ago) na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza
wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao
Tukio hilo limetokea Novemba 21,2014saa mb ili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake
wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth inayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa
madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited inayolinda mgodi huo ilipata taarifa kuwa kuna wachimbaji haramu maarufu kwa jina la
Wabeshi walitaka kuvamia mgodi wakiwa na silaha za jadi ikiwemo
mishale,mikuki,virungu,makombeo,mapanga na fimbo.
Kufuatia hali hiyo askari hao wa Zenneth walifika eneo la tukio kuwadhibiti Wabeshi hao lakini ghafla walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi
yakiwemo marungu,mishale,mikuki na
makombeo.
Baada ya kuona wanazidiwa nguvu,askari wa Zenneth walilazimika kuomba msaada wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) cha jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga.
Baada ya askari wa FFU kufika eneo la tukio nao walianza kushambuliwa na Wabeshi hao ,ndipo PC Idd akapigwa jiwe mdomoni kwa kutumia kombeo
na kung’oka meno sita mdomoni na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya
matibabu.
Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited Elisha Ndulu amethibitisha uwepo wa tukio hilo.
Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema Pc Idd alipigwa na kitu chenye ubapa mdomoni na kusababisha meno sita kung’oka na anaendelea kupatiwa matibabu,hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari wanawashikilia watu wanne kwa mahojiano zaidi na wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuwakamata wahusika wengine.
Chapisha Maoni