0
Aliyekuwa rais wa mpito nchi ya Zambia, Guys Scott.


Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani kwa kuvunja utaratibu wa katiba.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho. ''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya
chama,'' amesema Malozo Sichone.

Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo
ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.Scott
aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana.

Chapisha Maoni

 
Top