Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na
kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
Bunge TanzaniaKatika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato
wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya
viongozi.
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine
wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine
wa bodi.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na
kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi
wengine.
CHANZO:BBC
Chapisha Maoni