Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account, kuna mtu au kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya mtandao wa Twitter kwa jina la Edward Ngoyai
Lowassa, @edwardlowasa.
Kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea
bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Mhe. Lowassa.
Tunawaomba wananchi kupuuza yote
yanayoandikwa katika ukurasa huo. Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma,tutumie mitandao hiyo
kwa kuhamasisha maendeleo, amani, umoja na mshikamano kwa taifa letu.
Imetolewa na ofisi ya
Mh Edward Ngoyai Lowassa(Mbunge)
Chapisha Maoni