0
Jopo la majaji katika mji wa Ferguson katika jimbo la Missouri litakutana kwa mara nyingine leo Jumatatu Novemba 24, siku 108 baada ya kifo cha Mike
Brown. Mvulana huyo mweusi, ambaye hakua na silaha, aliuawa na askari polisi mzungu Agosti 9 mwaka 2014.

Machafuko yenye misingi ya kikabilia yaliibuka baada ya tukio hilo.
Uamuzi kuhusu kufunguliwa mashitaka au la dhidi ya Darren Wilson unatarajiwa kutolewa katika hali ya wasiwasi ambayo inaendelea kushuhudiwa ktaika mji wa Ferguson nchini Marekani, lakini hakuna matumaini yoyote kuwa jopo hilo la majaji litakua tayari kutoa uamzi wiki hii. 

Likizo za mwezi Novemba ziligubikwa na na maandamano mbalimbali ya wanafunzi katika mji wa Ferguson wakidai mwanga kuhusu kifo hicho. 

Shule zimefungwa tangu jana Jumapili na leo Jumatatu Novemba 24. Mkuu wa jimbo la Missouri ametangaza hali ya tahadhari.
Kikosi maalumu cha upelelezi cha Marekani FBI kimewatuma maafisa wake katika mji wa Ferguson, huku mashirika ya kiraia yakiwatuma wanasheria, wakati ambapo huenda kukatokea machafuko baada ya serikali ya jimbo la Missouri kupiga marufuku
maandamano ya aina yoyote.

Baba mzazi wa kijana huyo mweusi aliyeuawa, Mike Brown amewatolea wito vijana wa mji wa Ferguson
kuwa watulivu. " Mwanangu aliuawa biala hatia, kwa hiyo sintopendelea vijana waendelee kuawa bila hatia,
lakini kifo cha mwanangu kiwe ni mfani mzuri kwa kuleta mabadiliko ya kweli, mabadiliko ya amani", amesema mzazi wa kijana huyo mweusi, Mike Brown, ambaye jina lake linafanafa na la mwanae.

Chapisha Maoni

 
Top