0
MABINGWA wa England wako hatarini
kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya,
kufuatia usiku wa kuamkia leo kuchapwa mabao 2-1 Uwanja wa Etihad na CSKA Moscow katika mchezo wa Kundi E.

Mabao ya mshambuliaji wa CKSA Moscow, Seydou Doumbia dakika ya pili na 35 ndiyo yaliwapa wageni pointi tatu zote za mchezo huo, huku bao pekee la City likifungwa na Yaya Toure dakika ya nane.

Kocha Manuel Pellegrini alijikuta katika usiku mbaya mbaya zaidi baada ya wachezaji wake wawili, viungo Fernandinho na Toure kutolewa kwa kadi nyekundu hivyo kubaki na
wachezaji tisa uwanjani.

City sasa inashika mkia katika kundi hilo, kwa pointi zake mbili baada ya kucheza mechi nne, wakati Roma na CSKA zina pointi nne kila moja na vinara, Bayern Munich wana pointi 12 baada ya usiku huu kuichapa Roma. City watasafiri kuwafuata Roma katika mchezo wa mwisho wakitoka kuikaribisha
Bayern Munich katika mchezo ujao.

Kikosi cha Man City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Jesus Navas/ Nasri dk46, Toure, Fernando/Dzeko dk65, Milner, Aguero na Jovetic/Fernandino dk46.

CSKA Moscow; Akinfeev, Mario Fernandes, V Berezutski, Ignashevich, Schennikov, Musa, Wernbloom, Natcho, Dzagoev, Eremenko na Doumbia/Milanov dk67.

Chapisha Maoni

 
Top